Wizara ya usalama imebaini kuwepo kwa maafisa wa polisi, ambao hushurikiana na wahalifu katika kuendeleza mashambulizi na wizi, wa za mali ya wananchi wa maeneo yanayo kabiliwa na ukosefu wa usalama nchini.
Kulingana na waziri wa Usalama nchini Kipchumba Murkomen, baadhi ya wahalifu wamekuwa wakipewa risasi na maafisa wa polisi, wanaoshika doria katika maeneo hayo.
Akizungumza katika kikao na wanahabari kule Mjini Eldoret Kaunti ya Uasin Gishu, waziri Murkomen amesema kuwa maafisa hao watakabiliwa kisheria.
Waziri huyo amesema kuwa idara ya usalama imelazimika kubadilisha shughuli za uchunguzi dhidi ya visa vya uhalifu, kwa kile anachosema wakati mwingi wahalifu, wamekuwa wakikamatwa huku wanaofadhili vitendo hivyo wakikosa kuchukuliwa hatua zozote za kisheria na hivyo kukithiri kwa visa hivyo.

