Waziri wa leba nchini Alfred Mutua amewaonya vijana wanaopata nafasi za ajira mataifa ya nje, dhidi ya kujihusisha na visa vya utovu wa nidhamu, wanapokuwa kazini kule ughaibuni.
Kulingana na waziri Mutua, huenda hatua hiyo, ikawasababisha kufutwa kazi na hata kufutiliwa mbali kwa kandarasi zao, sawia na kukabiliwa kisheria.
Akizungumza katika kaunti ya Kwale, amesema kuwa kuna baadhi ya vijana ambao tayari wamerudishwa humu nchini, kufuatia visa vya utovu wa nidhamu miezi michache baada yao kunufaika na kazi hizo.
Akigusia swala la utumizi wa mihadarati waziri Mutua aidha amewataka vijana hao, kukomesha utumizi wa mihadarati kwani hakuna taifa linaloshabikia uraibu.

