Aliyekuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagwa amemkashifu rais William Ruto kwa madai ya kutumia vijana, kutatiza mikutano yake ya kisiasa.
Kwa mujibu wa Gachagwa, amekuwa akishuhudia makabiliono kati ya maafisa wake binafsi wa usalama na vijana ambao wamekuwa wakivamia mikutano yake, jambo ambalo ametaja kutoka kuwa sawa.
Akizungumza katika kanisa la PCEA Kasarani kaunti ya Nairobi, baada ya vijana kuvamia kanisa hilo na kusababisha vurugu kabla ya kudhibitiwa na maafisa wake wa usalama, Gachagwa ameibua madai ya Rais William Ruto, kushirikiana na gavana wa kaunti ya Nairobi, Johnson Sakaja katika kufanikisha vurugu hilo.
Vile vile ameibu madai ya maafisa wa polisi, kuagizwa kutofika katika eneo la tukio, ili kuweka usalama wakati kulipo shuhudiwa vurugu hilo.

