MABWENYENYE WALIONYAKUA ARDHI KATIKA FUO ZA BAHARI KAUNTI YA KWALE WAKABILIWA KISHERIA.

Waziri wa madini na uchumi wa bahari na maziwa nchini Hassan Joho, ametoa agizo la kuondolewa kwa mabwenyenye walionyakua ardhi za fuo za bahari kaunti ya Kwale, kwani walikiuka cha sheria za umiliki wa ardhi.

Waziri Joho  amezitaka afisi za kamishna wa Kwale, wizara ya ardhi ,shirika la KWS  na ile ya mazingira  NEMA, kutumia sheria zilizopo, kuwafurusha mabwenyenye waliojenga   katika  ardhi  za  ufuoni,  ili kutoa nafasi kwa wavuvi   kufanikisha shughuli zao za  kiuchumi.

Wakati uohuo ameitaja kaunti ya Kwale kufaidika na miradi mikubwa ya maendeleo kutoka kwa serikali ya kitaifa.

Waziri  Joho ameyasema haya wakati wa kuzindua ujenzi wa  mradi wa jumba la  kisasa,  la kuhifadhi samaki almaarufu  Mwaepe fishing landing site huko Msambweni  kaunti ya  Kwale, ujenzi unaofadhiliwa na benki kuu ya dunia, kwa gharama ya shilingi milioni 256.