ASKOFU MARTIN KIVUVA ASHINIKIZA MALIPO YA MADENI YA HOSPITALI ZA KIBINAFIS NCHINI.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki eneo la Pwani, Martin Kivuva ametoa wito kwa serikali kuu, kutatua changamoto zinazo kabili wakenya wanaotumia bima ya matibabu SHIF, inayotekelezwa na mamlaka SHA, kupitia idara ya afya.

Kivuva amesema kuwa, wakenya wengi wamekuwa wakiaga dunia huku wengine wakiendelea kupitia hali ngumu za kiafya, kutokana na ukosefu wa matibabu, kwani wanatagemea bima hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria misa ya jumatano ya majivu katika kaunti hiyo, askofu Kivuva amesema kuwa wadau wa mamlaka ya SHA, wanapaswa kuwajibika katika kutatua changamoto za bima ya SHIF, ili wakenya wanufaika na huduma za matibabu.

Vile vile Kivuva amesisitiza haja ya serikali, kulipa hospitali za kibinafsi malimbilizi ya madeni yaliyokosa kulipwa na bima ya awali ya NHIF, wakati wanapo wanapoendeleza kampeni ya wakenya, kujisajiliwa kwa bima mpya.