SENETA WA KAUNTI YA NANDI, SAMSON CHERARKEY APONGEZA USHURIKIANO WA RAILA ODINGA NA RAIS WILLIAM RUTO.

Baadhi ya wandani wa rais William Ruto kwenye bunge la seneti wamepigia upatu ndoa ya Raila Odinga na kiongozi wa taifa.

Wakiongozwa seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherarkey, amesema kuwa hatua ya serikali ya Kenya kwanza kuwateua baadhi ya viongozi wa ODM kwenye baraza la mawaziri nchini ni ishara kuwa muungano huo utafaulu.

Seneta huyo aidha ameelezea kuwa na imani ya Raila Odinga kumuunga mkono rais William Ruto, katika kuwania wadhifa wa urais mwaka 2027.

Vile vile Cherarkey amewakashifu vikali viongozi wa upinzani huku akisema kuwa, hawana uwezo wa kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Ikumbukwe kwamba seneta huyo pia awali alikuwa amewasilisha mswada wa kuongezwa kwa muhula wa rais kuhudumu.