MZOZO KATI YA KAMPUNI YA CHUMVI ENEO BUNGE LA MAGARINI KAUNTI YA KILIFI NA MAMLAKA YA MAJI NCHINI WAZUA HOFU KATI YA WANANCHI ENEO HILO.

Wito umetolewa kwa serikali kuu kuingilia kati kesi inayotishia kufungwa kwa kampuni ya chumvi katika wadi ya Gongoni eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.

Kulingana wananchi katika eneo hilo wakiongozwa na mwanaharakati wa kijamii Gabriel Shungu, pamoja Mwanasiasa Furaha Chengo Ngumbao, kampuni hiyo imesaidia wananchi wengi kukimu mahitaji yao na hivyo huenda jamii za eneo hilo, zikapita changamoto kuu ya kukimu mahitaji yao iwapo itafungwa.

Wakizungumza na wanahabari kwenye maandamano ya amani eneo hilo, wameeelezea haja ya viongozi wakuu kaunti ya Kilifi na kitaifa, kuingilia kati kesi ya kampuni hiyo na Mamlaka ya maji nchini, ambayo inatishia kusitisha shughuli za utendakazi wa kampuni hiyo.

Aidha, baadhi ya wananchi wamesema kuwa kuna haja yao kuhusishwa katika kesi hiyo, kwani licha kuwepo kwa makosa yanayo tekelezwa na kampuni hiyo, wengi wa wananchi katika eneo bunge hilo, wamenufaika pakubwa kiuchumi na mapato, kupitia kuwepo kwa kampuni hiyo ya chumvi.