Rais William Ruto amesema kuwa kuna haja ya taifa la Kenya kuwekeza zaidi katika elimu ya taaluma ambazo, huhitajika katika ajira za mataifa ya ulimwengu.
Kulingana na Rais, Kenya ina idadi kubwa ya watu walio na uwezo wa kufanya kazi mbali mbali ulimwengini na kwa mda sasa taifa hili, limekuwa likisifiwa kwa kuwa na wafanyakazi bora zaidi.
Akizungumza katika taifa la Misri, kwenye kikao na wakenya, kiongozi wa taifa amewaopongeza wakenya walioko inje ya taifa hili, kwa kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha uchumi wa Kenya.
Kwa upande wake naibu wa rais Profesa Kithure Kindiki, amesema kuwa jumla ya wakenya laki mbili, wamenufaika na mpango wa serikali kuwatafutia wananchi nafasi za ajira katika maitaifa ya ulimwengu.

