Rais William Ruto amewahakikishia wakenya kuwa ana nia ya kuwaunganisha viongozi na wakenya wote, kutoka matabaka mbali mbali katika taifa hili.
Kulingana na Rais Ruto, maendeleo ya taifa la Kenya hayawezi kuafikiwa iwapo, kutakuwa na tofauti za kikabila ama hata mirengo ya kisiasa kati ya wananchi.
Akizungumza katika eneo la Dagoreti kaunti ya Nairobi hapo jana, Kiongozi wa taifa ameelezea kuwa na utayari wa kushirikiana na viongozi wengine katika taifa hili, kwa malengo ya kuboresha uongozi wake.
Ruto aidha amepongeza juhudi za viongozi wa Azimio la Umoja One Kenya, kujiunga na serikali ya Kenya kwanza na kusema kuwa hatua hiyo ni njia bora zaidi, itakayo hakikisha kuwa ajenda za serikali tawala zinaafikiwa kwa wepesi zaidi.

