SPURS YAILAZIMISHA BRENTFORD SARE YA 2-2

Totenham Hotspers ya ligi kuu nchini Uingereza imerejea katika kipute cha ligi hiyo jioni ya leo katika mechi ya mapema na kupiga sare ya mabao 2-2 dhidi ya wananyuki Brentford.

Kiungo wa ujerumani Vitally Janelt ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwaweka mbele Brentford kabla ya Toney Ivan kuingia kimyani kwa goli la pili.

Hata hivyo nahodha ya Spurs Harry Kane alianza kwa kukomboa kabla ya Piere Hojberg kusawazishia vijana hao wa mkufunzi Antonio Conte.

Kwa matokeo hayo sasa Spurs ya mkufunzi Conte wanasalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama 30 wakati Brentford ikisimama katika nafasi ya tisa na alama 20.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *