Waziri wa elimu humu nchini Ezekiel Machogu amesema kuwa wanafunzi bora katika mtihani wa kitaifa wa KCPE ambao ni Lewis Otieno Omondi na Fwaro Makokha Robinson, wamemudu kupata jumla ya alama 431.
Akitoa matokeo hayo katika ukumbi wa mtihani house kule jijini Nairobi, waziri Machogu amesema kuwa wanafunzi zaidi ya milioni 1.2 walifanya mtihani huo huku wanafunzi 39 wanaoishi na ulemavu walimudu kupata alama 400 na zaidi.
Matokeo haya yametolewa kwa namna ya kipekee kwani waziri wa elimu hakuweka wazi wanafunzi kumi bora wala shule bora katika matokeo hayo kinyume na hali ilivyokuwa ikifanyika hapo awali.
Kwenye matokeo hayo pia Machogu amebainisha kuwa jumla ya watahiniwa 9,443 walipata alama mia nne na zaidi.
Aidha waziri huyo amesema kuwa matokeo ya mwaka huu sawia na yale ya mwaka ujao yatakuwa ni matokeo ya mwisho ya mtaala wa elimu wa 8-4-4

