BUNGE LA SENETI LAENDELEZA HOJA YA KUBANDULIWA KWA GAVANA WA KAUNTI YA MERU KAWIRA MWANGAZA.

Barua za mwaliko zinatarajiwa kutumwa kwa wote watakaowasilisha ushahidi dhidi ya kubanduliwa kwa gavana wa Meru kawira Mwangaza.

Hii ni baada ya seneti kuafikiana kubuni kamati maalum ya kutathmini kubanduliwa mamlakani kwa gavana huyo ambapo barua hizo za mwaliko zitaanza kutumwa kwa wote watakaofika mbele ya kamati hiyo kuwasilisha ushahidi.

Wahusika wote watakuwa na siku tatu kuwasilisha stakabadhi zao, tarehe 22, 23 na 24 huku pande zote mbili zikiratibiwa kukutana ana kwa ana mbele ya kamati hiyo tarehe 24 kabla ya likizo fupi ya siku mbili kwa minajili ya sherehe za krismasi.

Tarehe 27 ya mwezi huu wa disemba vikao vitarejelewa ambapo itakuwa zamu ya bunge la kaunti ya Meru kuwasilisha hoja zake kisha gavana Mwangaza atajitetea tarehe 28.

Baada ya hapo, kamati husika ya maseneta 11 itaandaa ripoti inayotarajiwa kuwasilishwa kwenye bunge la seneti tarehe 30 mwezi huu.