WIZARA YA USALAMA WA NDANI YA WEKA MIKAKATI YA MAAFISA WA USALAMA KUDUMISHA USALAMA.

Idara ya usalama humu nchini imetangaza kuweka mikakati kabambe ya kudumisha usalama wa wakenya, hasa msimu huu wa sherehe za krismasi.

Kwa mujibu wa waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki, ni kuwa tayari wameweka mikakati ya kudumisha usalama, katika barabara kuu ambazo wananchi wanatumia kusafiri mashinani.

Akizungumza na wanahabari ameelezea kuwa madereva watakao kuwa wakikiuka sheria za barabarani, watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Haya yanajiri baada ya waziri wa barabara nchini Kipchumba Murkomen, kulalamikia ongezeko la idadi ya ajali za barabarani hasa katika sekta ya bodabada.