Kamanda wa polisi Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi Jonathan Koech amewataka madereva kuwa waangalifu zaidi wakati huu wa sherehe za disemba ili kuepuka ajali za barabarani.
Koech pia amesisitizia wachukuzi wa umma kuhakikisha kuwa wanadumisha usalama wa abiria wao badala ya kuendekeza utovu wa nidhamu barabarani.
Kauli ya Koech imejiri baada ya watu watatu kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani iliyotokea eneo la chumani ajali iliyowapelekea watu watatu kuaga dunia manamo siku ya Jumanne wiki hii.
Watatu hao walikuwa kwenye pikipiki iliyogongana ana kwa ana na lori.

