Kaunti ya kwale ni miongoni mwa kaunti 23 nchini zitakazopokea chakula cha msaada kutoka kwa serikali ya kitaifa kwani kaunti ndogo za Lungalunga na Kinango kaunti hiyo zimetajwa kuathirika pakubwa na baa la njaa.
Haya ni Kwa mujibu wa gavana wa kaunti ya kwale Fatuma Achani alipozindiua mradi wa maji wa Nyalani-Mwangoni-Bang’a katika eneo la Kinango utakaogharimu shilingi milioni 159.
Achani amesema kuwa tayari mikakati imeidhishwa kufanikisha utoaji wa chakula hicho cha msaada kwa wananchi
Wakati uo huo Naibu Gavana Josephat Chirema Kombo amewatahadharisha wanaolenga kuuza chakula hicho cha msaada kuwa serikali itawakabili kisheria.

