Naibu kamishana eneo la Matuga kaunti ya Kwale Lucy Ndemo, amewaonya wananchi dhidi ya kuendeleza semi za chuki kwa viongozi waliochaguliwa eneo hilo.
Ndemo amesema kuwa wale wanaoendeleza semi za chiki mitandaoni, watakabiliwa kwa mujibu wa sheria kwani idara ya usalama, inaendeleza uchanguzi dhidi yao.
Amewataka wananchi kudumisha ushirikiano mwema kati yao na viongozi walioko serikalini, badala ya kuwakashifu na kuwatusi mitandaoni.
Haya yanajiri siku chache baada ya naibu wa gavana kaunti ya Kwale Chirema Kombo, kuibua madai ya kuwepo kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiendeleza semi za chuki mitandaoni, dhidi ya viongozi waliochaguliwa.

