MKURUGENZI MKUU WA IDARA YA UPELELEZI GEORGE KINOTI AMEJIUZULU.

Mkurugenzi mkuu wa idara ya upelelezi nchini DCI George Kinoti amewasilisha rasmi barua ya kujiuzulu katika nafasi hiyo ya uongozi.

Haya ni kwa mujibu wa rais Dktr William Kipchirchi Arap Samoei Ruto, ambaye amesema kuwa sasa idara ya polisi nchini inapaswa kuteua atakeshikilia nafasi hiyo, kabla ya kupata yule atakekabidhiwa nafasi hiyo rasmi baada ya watu kutuma maombi ya kupea  wafidha huo.

aidha ameongeza kuwa Mkuu wa Polisi Hillary Mutiambai ameomba kuenda mapumzikoni kwa mda, kutokana na hali yake ya afya na kumpendekeza Mhandisi Japhet Koome Nchebere, ambaye aliwakuwa kamanda wa polisi kaunti ya Nairobi kushikilia wadhifa wa Mutiambai.