zoezi la ugavi wa chakula kwa wenyeji wa Vigurungani laanzishwa kaunti ya Kwale

 

Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amesema serikali ya kaunti hiyo kwa ushirikiano na kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium imezindua ugavi wa chakula cha msaada kwa wenyeji wa Vigurungani katika eneo bunge la Kinango.
Mvurya ameipongeza kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo kwa wenyeji wa eneo hilo huku akiongeza kwamba tani 100 za mbegu zitagawanywa kwa wakaazi ili kuendeleza kilimo.
Wakati uo huo afisa wa jamii katika kampuni hiyo ya Base Titanium Pius Kassim amesema jumla ya Familia 4000 zimefaidika na msaada huo wa chakula na kusema ni chakula ambacho kitadumu kwa muda wa wiki 3 zijazo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.