ZAIRA YA RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU YA BORESHA UHUSIANO KATI YA KENYA NA TANZANIA.

Serikali ya Kenya imeweka sahihi mkataba kati yake na Taifa la tanzania, wa kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka kwa taifa la Tanzania, hadi Pwani mwa Kenya .

Akizungumza katika ikulu ya Rais hapa nchini Kenya Rais wa Tanzania Samia Suluhu hasaan amesema kuwa, tayari mataifa hayo yamekuwa yakiendeleza mazunguzo yatakayo fanakisha hatua za kutekeleza miradi hiyo, huku akisema kuwa ni njia mojawapo ya kuboresha sekta ya biashara kati ya Kenya na Tanzania.

Kuhusiana na swala la kucheleweshwa kwa madereva wanaoinga katika taifa hilo la Tanzania, kufuatia baadhi ya masharti yaliyokuwa yakiwekwa na taifa hilo, viongozi hao wamewataka mawaziri wa mataifa yote mawili, kuja pamoja na kuhakikisha kuwa wanarahisisha huduma za vipimo vya covid 19 mpakani.

Hata hivyo Rais Kenyatta ameongeza kuwa hatua ya mawaziri hao kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara, itahakikisha urahisi wa hudumu za usafirishaji wa bidhaa katika mataifa haya, na hivyo basi kukuza sekta ya biashara kwani idadi kubwa ya wawekezaji, watapata fursa ya kuwekeza.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.