YOUNG BULLS YAANZA LIGI KWA MATAO YA JUU, YAINYUKA RUIRU HOTSTARS MAGOLI 4-0

Vijana wa klabu ya Young Bulls ya kaunti ya Kilifi imeanza ligi kwa matao ya juu baada ya kuandikisha ushindi mnono wa magoli 4-0 mikononi mwa wageni Ruiru Hotstars Ya kaunti ya Kiambu kwenye mechi ya ligi ya kitaifa ya daraja la kwanza, BETKING DIV1 LEAGUE iliyochezwa kwenye dimba la Alaskan mjini Malindi.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na Tama La Spoti, mkufunzi wa klabu ya Young Bulls yenye makao yake eneo la Kwa Ndomo wadi ya Sabaki kaunti ndogo ya Malindi Billy Mwangemi amesema kwamba lazima timu ijipange kisawasawa ili kuandikisha matokeo mazuri ikitegemea kwamba wao ni limbukeni wa ligi hii.

”Fixture ilipotoka tulipata kwamba mechi yetu ilikuwa home na kwetu tukasema kwamba tutatumia fursa hiyo kama advantage. Tukajiandaa vizuri na game imeenda jinsi tulivyotaka,” alisema Mwangemi, ”Naweza sema congaratulations to the boys kwa kufanya kile tulipanga. Lazima mtu ujipange bila mtu kujipanga mazoezi tactical na vitu sawia na hivyo utajipata vibaya kwenye hii ligi so kwa upande wetu tulijipanga.”

Mwangeni aliongezea kwamba, ”Sisi letu ni kujikaza kwa kuwa ni mara yetu ya kwanza hatuwezi underrate any timu na tunajua sisi ni underdogs so lazima tujikaze zaidi. Underdogs kwa kuwa ni mara yetu ya kwanza na wapo ambao ni wakongwe wa ligi hii wanaoijua vizuri.”

Kwa upande wake maneja wa timu ya Ruiru HotStars ni kuwa mchezo ulikuwa mzuri na wa haki na wamejifunza kutokana na makosa waliyofanya.

‘’Kwa mechi kuna results tatu. Kuna win, draw na lose. Kwa leo tumelose, so the best thing saa hii ni how tutamove on. Venye umeanguka si mhimu vyenye utainuka na venye utainuka haraka na kumove on ndio muhimu zaidi. Game ilikuwa fare. Niseme tu ilikuwa bad day kwa upande wetu tumekubali tumepoteza in a clean way,’’ alisema meneja wa timu ya Ruiru HotStars Kariuki Gideon.

MATOKEO MENGINE

Dummen Orange 1-1 Congo Boys (Embu)

Liberty Sports 2-1 SS Assad (Gems Ambridge School Nairobi)

3 thoughts on “YOUNG BULLS YAANZA LIGI KWA MATAO YA JUU, YAINYUKA RUIRU HOTSTARS MAGOLI 4-0”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.