WIZARA YA FEDHA YAZIONYA TAASISI ZA SERIKALI

Taasisi za serikali zimepatiwa siku 20 kukamilisha kulipia madeni ambayo zinadaiwa .

Akizungumza bungeni wakati wa kuwasilisha bajeti ya mwaka wa kifedha 2021/2022, waziri wa fedha nchini Ukur Yatani Kanacho ameonya kuwa huenda wizara yake ikalazimika kusitisha kutuma fedha zaidi kwa taasisi hizo ikiwa hazitaheshimu agizo.

Amesema kuwa taasisi za serikali kuu pamoja na zile za kaunti zinadaiwa madeni ya thamani ya mabilioni ya fedha hali ambayo imesababisha kwa baadhi ya biashara kufungwa hivyo kuathiri uchumi.

Mwezi wa Aprili mwaka huu waziri huyo wa fedha alikuwa ametao onyo kuwepo kwa madeni katika taasisi hizo za serikali ambapo aliziagiza yalipwe  kabla ya mwezi huo lakini hili halijafanyika hadi kufikia sasa.

Katika bajeti hiyo ya Shilingi bilioni 142 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha ajenda nne kuu za serikali, shilingi  bilioni 121 zimetengwa kwa ajili ya wizara ya afya na kusema kuwa kodi imeondolewa kwa bidhaa za afya zitakazoingia nchini kama vile dawa za kuzuia madhara ya homa, dawa zinazotumika kuongeza nguvu mwilini sawia na mashini za kusaidia kupumua.

Waziri huyo amesema kuwa wanaotengeneza bidhaa za afya nchini watapunguziwa bei ya mali ghafi ili kufanikisha biashara zao.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.