WITO WATOLEWA KWA SERIKALI KUFUNGUA KAUNTI 5 ZILIZOFUNGWA

Afisa wa Maswala ya dharura katika shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini la Haki Afrika Mathius Shipetta ameitaka serikali kuzifungua kaunti 5 zilizofungwa hivi majuzi kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona ili kutoa nafasi za ibada kwa waumini wa dini ya kiislamu wanaomini kuwa mtukufu wa Ramadhan.
 
Shipeta amesema kumeshuhudiwa kupungua kwa maambukizi ya virusi vya Corona katika kaunti hizo 5 na ni haki kwa waumini wa dini hiyo kwenye kaunti hizo kupewa fursa ya kufanya ibada zao kama wenzao katika kaunti zingine nchini.
 
Aidha Shipeta amewataka wananchi kuzidi kuzingatia maagizo ya serikali ya kudhibiti msambao wa virusi vya Corona.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.