Msimamizi wa kituo cha matibabu cha Kijanaheri eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Manyara Nyakea amewahimiza Wakenya kujisajili kwenye bima mpya ya afya ya SHA.
Akizungumza huko Shomela katika zoezi la kuwasajili wenyeji kwenye bima hiyo, Nyakea amesema ni bora zaidi kwani itaweza kuwasaidia wale ambao wanaugua magonjwa sugu kama ugonjwa wa saratani kupata matibabu.
Nyakea amesema Wakenya wengi wamekuwa na dhana potofu kuhusu bima ya SHA kutoka kwa wale wanaoipinga na kusisitiza umuhimu wa watu kujisajili.
Wakati huohuo, Nyakea amesema wanaendelea kutoa matibabu ya bure kwa wenyeji wa Shomela ambayo yameratibiwa kukamilika siku ya Jumamosi na kuwahimiza wakazi kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma kama kupima ugonjwa wa saratani miongoni mwa mengine.