Wenyeji wa Kwale walalamikia fidia

 

Wakaazi wa vijiji vitatu katika kaunti ya Kwale wanalalamikia kupewa fidia kutokana na mradi wa barabara ya Dongo Kundu kwa kile wanachodai kuwa awamu ya pili ya mradi huo umewasababishia kupoteza makao.
Wakaazi hao wamesema kuwa serikali imekuwa ikiwashinikiza kutoa stakabadhi halisi za kumiliki ardhi hiyo kabla ya kupewa fidia ila hilo halijaafikiwa kwani wamedai kuwa ardhi hizo ni za babu zao.
Haya yanajiri siku chache baada ya mamlaka ya usimamizi wa bara bara kuu nchini KENHA kutoa shilingi milioni 120 zitakazotumika kuwafidia wenyeji watakaoathirika na mradi huo wa Dongo Kundu.
Pesa hizo zimekabidhiwa tume ya ardhi nchini na kinachosubiriwa ni uchunguzi kufanywa ili khakikisha waathiriwa halisi wanapokea pesa hizo.
Awamu ya pili ya mradi huo inaendelea ikitarajiwa kuchangia pakubwa katika uchumi na kurahisisha uchukuzi.
Ni mradi ambao umefadhiliwa na serikali ya Japan kwa takribani shilingi bilioni 24 huku wenyeji wakitarajia kupata ajira.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.