WELDON KORIR NA AGGREY MUCHELULE WAKOSA KUTEULIWA NA RAIS UHURU KENYATTA

 

Rais Uhuru Kenyatta anazidi kupata shinikizo kutaja sababu za kutowateua majaji 4 ambao walipendekezwa na tume ya huduma za mahakama JCS kuhudumu katika mahakama ya Rufaa.

Miongoni mwa majaji 4 hao ambao 2 ni Jaji Joel Ngugi na George Odunga walikuwa miongoni mwa Jopo la majaji 5 wa mahakama kuu walioharamisha mchakato wa BBI uliopania kuifanyia Katiba marekebisho.

Kenyatta hakuwateua Weldon Korir na Aggrey Muchelule kuwa majaji wa mahakama ya Rufaa na kuyarejesha majina yao kwa tume ya huduma  za mahakama JSC bila kutoa sababu zozote hali ambayo imeibua hisia mseto.

Katika kuidhinishwa kwa  uteuzi wa majaji 41 waliokuwa wamependekezwa na JSC rais hakuidhinisha uteuzi wa Makori Evan Kiago na Judith Omange Cheriyot kwa madai hawakuafikia vigezo hitajika na kuwaidhinisha majaji 34.

Majaji 9 kati ya 34 wanatarajiwa kufanya kazi katika mahakama  na baadhi ya majaji walioteuliwa ni Msagha Mbogoli, Hellen Omondi, Mumbi Ngugi, Francis Tuiyot, Pauline Nyamweya na jaji Jessie Lessit miongoni mwa majaji wengine.

Hatua hiyo ya rais inadaiwa kuwa njama ya kulipiza kisasi huku ikizidi kukosolewa na kusemekana itazidisha uhasama baina serikali tendaji na idara ya mahakama.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.