Waziri wa madini na raslimali za baharini na maziwa nchini Salim Mvurya ametoa makataa ya hadi mwezi Disemba mwaka huu wa 2023, kwa mkandarasi ambaye alikabidhiwa ujenzi wa kiwanda cha samaki cha Liwatoni kaunti ya Mombasa kukamilisha kwa awamu ya Kwanza.
Akizumgumza katika kaunti hiyo alipozuru kiwanda hicho amesema mradi huo ambao unagharimu kima cha shilingi bilioni 1.4 utaweza kubuni nafasi za ajira zaidi ya elfu 3 za moja kwa moja, ujenzi wa kiwanda hicho kitakapokamilika.
Mvurya amesema hapo awali mradi huo ulikosa kukamilishwa kwa wakati kutokana na uhaba wa fedha japo kwa sasa, serikali imetenga fedha za kutosha ili kuukamilisha.
Wakati huohuo amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuhifadhi tani zaidi elfu moja ya Samaki na kitasaidia kwa asilimia kubwa kuimarisha sekta ya uvuvi.
Vilevile, Mvurya amesema serikali kuu imewekeza vilivyo katika miradi mbalimbali ambayo inafungamana na sekta ya uchumi unaohusiana na bahari ili kuboresha sekta hiyo kulingana na Ajenda ya serikali ya Kenya Kwanza.
SALIM MVURYA ATOA MAKATAA YA HADI MWEZI DISEMBA
