WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAHIMIZWA KUZINGATIA MASHARTI YA KUDHIBITI CORONA

Gavana wa Kwale Salim Mvurya amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuzingatia masharti ya kudhibiti msambao wa korona wakati huu ambapo wanaendeleza siku kuu ya idd ul adha.
Mvurya amesema kuwa hakuna anayeruhusiwa kukiuka masharti ya kudhibiti corona kwa kisingizio cha kusherehekea idd akisema kuwa wale watakiuka sheria hizo watakabiliwa kisheria.
Gavana huyo amesisitiza haja ya jamii kusaidiana miongoni mwao kupitia misaada ya chakula, mavazi miongoni mwa mahitaji mengine ya kimsingi.
Naye sheikh wa msikiti wa Kongo kule Diani kaunti ya Kwale ameisihi idara ya usalama kuwajibika katika kudhibiti visa vya watu kutekwa nyara na kupotezwa katika hali tatanishi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.