Watu watatu wapoteza maisha katika ajali mbaya ya barabarani

 

Watu watatu wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 20 wakijeruhiwa vibaya baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani iliyotokea katika eneo la Gede kwenye barabara kuu ya Malindi kuelekea Mombasa kaunti ya Kilifi.
Akithibitisha ajali hiyo, kamanda wa trafiki mjini Malindi kaunti ya Kilifi George Naibei amesema ajali hiyo ilihusisha gari dogo la kibinafsi na Matatu ya abiria baada ya magari hayo kugongana ana kwa ana ambapo Matatu ilikuwa ikielekea Mombasa huku gari dogo likija mjini Malindi.
Naibei amesema kuwa gari hilo dogo aina ya Wish lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi kabla ya kushuhudiwa kwa ajali hiyo na kuwataka madereva wote wa magari ya uchukuzi wa umma kuwa waangalifu zaidi kila wanapokuwa barabarani.
Kwa upande wake, msimamizi wa hospitali kuu ya Malindi Evans Ogato amesema majeruhi wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali hiyo huku walioaga dunia miili yao ikihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Malindi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.