Wasichana watatu 3 mbaroni kwa kuchafua picha ya Rais

Wasichana watatu nchini Burundi, wanazuiliwa jela wakisubiri kuhukumiwa Mahakamani baada ya kufutafuta picha ya rais Pierre Nkurunziza kwenye vitabu vya kusoma.

Imeelezwa kuwa wasichana hao wana umri wa miaka 15, 16 na 17 na iwapo watapatikana na kosa la kumdhihaki rais, atafungwa jela miaka mitano.

Majaji wamesema kuwa wasichana hao ni lazima wafunguliwe mashtaka kwa kosa hilo, na kuagiza wazuiwe kwenye jela ya watoto mjini Ngozi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wasichana hao wamekuwa wakizuiwa tangu tarehe 12 mwezi Machi, baada ya kukamatwa pamoja na mvulana mwenye umri wa miaka 13 ambaye baadaye aliachiliwa huru.

Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali ndio inayoshughulikia kesi hii, na haijafahamika ni lini kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa mujibu wa Lewis Mudge, mwanaharakati kutoka Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la  Human Rights Watch.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.