Wanyama kujiunga na klabu ya Galatasaray

Siku nne baada ya kipindi kirefu cha uhamisho nchini Uingereza kufungwa Agosti 8, ripoti kutoka nchini Uturuki zinasema kuwa mmoja kati ya viungo wakabaji Mkenya Victor Wanyama anayechezea timu ya Tottenham Hotspur na Mfaransa Tiemoue Bakayoko kutoka Chelsea wako kwenye rada ya Galatasaray.

Tovuti ya Sport Witness inasema kuwa afisa kutoka Galatasaray, Sukru Haznedar yuko jijini London kwa mazungumzo.

Kocha Mauricio Pochettino alipendezwa na soka ya Wanyama na kumleta Southampton mnamo Julai mwaka 2013 na kisha Tottenham Juni mwaka 2016.

Hata hivyo, baada ya nahodha huyo wa Harambee Stars kukosa kucheza mechi nyingi kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya magoti katika msimu hiyo miwili iliyopita, kocha huyo kutoka Argentina alionyesha kumshiba Wanyama aliposaini viungo Tanguy Ndombele na Giovani Lo Celso.

Tovuti ya Sport Witness nchini Uturuki inasema, mmoja kati ya Wanyama ama Bakayoko atajiunga na miamba wa Galatasaray.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.