WANDANI WA NAIBU WA RAIS DAKTARI WILLIAM SAMOEI RUTO KUKUKUTANA LEO KAREN

Naibu wa Rais Daktari William Samoei Ruto anatarajiwa leo kukutana na wandani wake kujadiliana na kisha kutoa msimamo wao ikiwa wataunga mkono ripoti ya BBI au La.

Ni mkutano ambao umeratibiwa kufanyika nyumbani kwake huko Karen jijini Nairobi na inadaiwa kuwa tayari Maseneta na wabunge sambamba na viongozi wote wanaopinga BBI wamealikwa kwenye mkutano huo.

Ruto amekuwa akiwaongoza wandani wake kushinikiza baadhi ya marekebisho ya muswada anasema kuwa kungali na nafasi ya kupata mwafaka kuhusu baadhi ya ampendekezo ambayo wanahisi kuwa hayakushughulikiwa kama inavyopaswa.

Katika taarifa yake hapo jana katika kaunti ya Nakuru alisisitiza kuwa hakuna anayepinga marekebisha ya katiba japo kuna baadhi ya watu ambao wanashinikiza kuwepo kwa makundi mawili hasimu katika mchakato mzima wa BBI.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.