WANAOTUMIA MITANDAO VISIVYO KUKABILIWA KISHERIA

Licha ya Bodi ya kudhibiti ubora wa filamu nchini KFCB kutoa onyo kali kwa wanaotumia mitandao visivyo, bado kunadaiwa kuwa kuna wale ambao wangali wanaitumia katika mambo ambayo hayana maadili.
Akiongea kwenye kaunti ya Mombasa afisa mkuu wa bodi nchini Dr. Ezekiel Mutua amesema serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watakaokiuka maagizo ya bodi hiyo hususan msimu huu ambao wanafunzi wako nyumbani kwa likizo baada ya kufungwa kwa shule.

Mutua amewaonya wasanii dhidi ya kutumia mitandao visivyo ikiwemo kuonyesha filamu zinazokiuka sheria za mitandao ya kijamii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.