Wanaotumia kivuko cha Ferry cha Likoni Mombasa watahadharishwa

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo amewahimiza wanaotumia kivuko cha Ferry cha Likoni kufunika modomo na pua kwa kutumia kitambaa au barakoa kabla ya kuabiri Ferry eneo hilo.
Kulingana na Kitiyo amesema ni sharti agizo hilo lizingatiwe na watakaosalia midomo yao wazi au kushindwa kufunika pua zao hawataruhusiwa kuabiri Ferry hizo.
Kitiyo amesisitiza kwa wenyeji kusalia nyumbani huku kaunti hiyo ikiorodheshwa kuwa miongoni mwa kaunti zilizoko katika hatari ya kushuhudia maambukizi ya virusi vya Corona.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.