WANAKANDARASI WA UJENZI WA JUMBA LA MAMLAKA YA UBAHARIA WATAKIWA KUFIKA MBELE YA KAMATI YA BUNGE LA KITAIFA LINALO HUSIKA NA UWEKEZAJI

Kamati ya bunge la kitaifa inayohusika na masuala ya uwekezaji PIC ikiongozwa na mwenyekiti wake aliyepia mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir imemtaka mwanakandarasi aliyepewa kandarasi ya ujenzi wa jumba la Mamlaka ya Ubaharia nchini KMA kufika mbele ya kamati hio kuelezea jinsi fedha za kandarasi ya ujenzi huo zilivyotumika.

Hii ni kutokana na kuwa mwanakandarasi huyo amedaiwa kukwepa vikao vingi vya ukaguzi  vinayoandaliwa na kamati ya uwekezaji PIC kule Mombasa kuthathmini matumizi ya pesa katika mamlaka hio.
Kulingana na kamati hio mwanakandarasi huyo hapo awali alishindwa kuhudhuria kikao kwa kizingio cha kuhofia maradhi ya Covid-19.
Akizungumza kwenye kikao na bodi ya mamlaka ya KMA mjini Mombasa ,mwenyekiti wa kamati hio ya uwekezaji katika bunge la kitaifa Abdulswamad Shariff Nassir amesema ni muda mrefu mamlaka hio imekuwa haiweki wazi jinsi inavyofuja mamlioni ya pesa za umma.

Hii ni kutokana na kuwa mamlaka hio ikiongozwa na mkurugenzi wake Robert Mutegi Njue haitoi vitibitisho na stakabadhi ambazo kamati hio ya bunge inahitaji.

Hata hivyo kamati hio sasa imetoa muda wa siku nne ambapo ni siku ya jumatano kwa mamlaka hio ya KMA  kuwasilisha stakabadhi zote hitajika kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.

Aidha wafujaji wa pesa kwenye mamlaka hio watafichuliwa na kamati hio pindi tu uchunguzi kamili utakapo kamilika kama inavyofanya kwa kampuni zengine.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.