WANAFUNZI ENEO BUNGE LA MALINDI WANUFAIKA NA UFADHILI WA MASOMO YA SEKONDARI

Takriban wanafunzi 15 waliopata alama 350 na zaidi katika Wadi ya Kakuyuni eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi, watanufaika na mpango wa serikali ya kaunti wa kugharamia masomo yao ya shule ya upili.

Kulingana na Mwakilishi Wadi wa Kakuyuni Nixon Mramba, mpango huo umekuwa ukigharimu zaidi ya Millioni tatu kwa mwaka, kwa kuwalipia karo ya kila mwaka wanafunzi waliofanya vyema zaidi eneo hilo.

Akizungumza baada ya kupokea wanafunzi watakaoingia katika mpango huo, Mramba amedokeza kuwa serikali ya kaunti inalenga kupiga vita umaskini miongoni mwa jamii, kwa kupatia kipaumbele maswala ya elimu.

Kwa upande wao, Cornelius Kahindi Karisa na Dena Karisa Wyclife, wameelezea matumaini ya kutimiza ndoto zao kupitia ufadhili huo, wakidai hawakuwa na matumaini ya kujiunga na shule ya upili, kutokana na hali ya uchochole katika familia zao.

Mama ya watoto hao kwa jina Mapenzi Karisa Katana amesema amelazimika kuuza mboga, kwa zaidi ya miaka 6 kusomesha watoto hao baada ya baba yao mzazi kuaga dunia.

Eneo hilo lina jumla ya wanafunzi 66 ambao wanaendelea kunufaika na ufadhili huo, tangu ulipoanzishwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.