WALIMU WAKUU WA SHULE ZA UMMA NCHINI WAPONGEZWA

Katibu wa chama cha walimu cha KNUT tawi la Kilindini katika kaunti ya Mombasa Dan Aloo amepongeza juhudi za walimu wa shule za umma baada ya shule hizo kutangazwa kama shule zilizo nakili matokeo bora katika mtihani wa kitakifa wa KCPE.

Akizungumza na kituo hiki Aloo ametaja hatua ya serikali kuweka mikakati kabambe iliyo wekwa na serikali kuu katika kuhakikisha kuwa watoto katika shule za umma wanapata vitabu vya kufanya masomo ya ziada na marudio na hata agizo la kutofukuzwa shuleni licha ya kutokuwa na karo kuchangia pakubwa katika matokeo mazuri ya mtihani huo.

Katibu huyo amewapongeza wanahabri nchini kwa kile alichosema kuwa walikua katika msatari wa mbele kuwahimiza wazazi kuwachukua jukumu la kuwatunza watoto hasa pale walipokuwa majumbani mwao kufuatia hatua ya ongezeko la virusi vya Korona vilivyo pelekea kutangazwa kwa hatua ya kufungwa kwa taasisi za elimu nchini.

Aidha Aloo ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa na mashirika kujitokeza na kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliokuwa na matokeo bora katika mtihani huo wanajiunga na shule za upili na hata kupata ufadhili kutoka kwa mashirika ya kijamii na wahisani.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.