VISA VYA WANAOJITIA KITANZI VINADAIWA KUCHANGIWA NA MSONGO WA MAWAZO

Ogezeko la idadi ya Visa vya watu wanaoripotiwa kijitia kitanzi nchini imechangiwa na hatua ya watu kukumbwa na msongo wa mawazo kufuatia baadhi ya matatizo ambayo hukumba binadamu.
Haya ni kwa mujibu wa Monica Kamau muuguzi anayehusika na matibabu ya watu walio na matatizo ya akili katika hospitali moja mjini a Malindi ambaye amesema kuwa moja wapo ya dalili za mtu kukumbwa na msongo wa mawazo ni kubadilika kwa tabia jambo ambalo huathiri utendakazi wake wa kawaida.
Hata hivyo Monica amelalamikia hatua ya watu kupuuza matibabu ya watu walio matatizo ya akili kwa kile anachokidai kuwa wengi wao hawana ufahamu kuhusiana na ugojwa huo jambo ambalo hupelekea ongezeko la madhara kwa mgonjwa.
Aidha, wamewashauri wananchi kuchukua hatua ya kufika katika vituo vya afya iwapo watagundua mtu kuwa na dalili sawia na zile za mtu kusongwa na mawazo ili kushauriwa kabla ya kuongezeka kwa madhara zaidi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.