VISA VYA UKEKETAJI VINAZIDI KUONGEZEKA KAUNTI TA TAITA TAVETA

Shirika la sauti ya wanawake kaunti ya Taita Taveta limeeleza ongezeko la visa vya ukeketaji wa wasichana wadogo katika maeneo ya kaunti hiyo.
Mwenyekiti wa shirika hilo, Makrina Mwamburi amewaelekezea kidole cha lawama baadhi ya wazazi wa kike akisema kuwa wanachangia katika kuendelezwa kwa ukeketaji miongoni mwa wasichana.
Makrina amesema kuwa eneo ambalo linaaminika kuendeleza ukeketaji ni eneo la Taveta ambapo wasichana hutoroshwa hadi nchi jirani ya Tanzania kufanyiwa uovu huo.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa kuna haja ya maafisa tawala kushirikiana na idara ya usalama kwa lengo la kuzuia wanafunzi kuvukishwa katika taifa hilo jirani ili kukeketwa kabla ya kurejeshwa humu nchini.
Makrina amesema kuwa kutokana na mikakati thabiti iliyowekwa nchini imewafanya wakeketaji hao kukimbilia Tanzania ambapo wanatekeleza ukeketaji kwa wasichana wadogo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.