Visa vya mauaji ya wazee kwa shutuma za uchawi vimepungua Kilifi

 

Idara ya usalama imethibitisha kuwa visa vya mauaji ya wazee kwa shutuma za uchawi vimepungua kwa kiasi kikubwa kaunti ya Kilifi.
Akizungumza mjini Kilifi kamanda wa polisi,James Mugera amehoji kuwa hilo limeafikiwa kufuatia hamasa za mara kwa mara zilizokuwa zikiendelezwa mashinani.
Mugera sasa amesema ni sharti jamii iwashirikishe washauri mbalimbali kuleta mwafaka wa migogoro ya kifamilia bila kutekeleza mauaji.
Aidha, ameitaka jamii hasa vijana kukoma kutekeleza uhalifu uo kwani wazee wanahaki ya kuishi kama binadamu wengine.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.