VIONGOZI WATAKIWA KUHAMASISHA WNYEJI WA KAUNTI YA KILIFI KUHUSU USAJILI WA WAPIGA KURA

Kiongozi wa vijana kaunti ya Kilifi Fikirini Jacobs, anawataka viongozi mbalimbali kufanya vikao ili kuwaelimisha wakazi kuhusu umuhimu wa kusajiliwa kuwa wapiga kura.

Kulingana na Jacobs watu wengi hawajitokezi kusajiliwa kuwa wapiga kura kutokana na kile ambacho, anadai kuchangiwa na ukosefu wa hamasa.

Jacobs amesema huu sio wakati wa kufanya siasa za uchaguzi na kusema ameanzisha ziara ya kuzuru sehemu mbalimbali kaunti ya Kilifi, kuhamasisha watu kusajiliwa kuwa wapiga kura ili kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2022.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mwaniaji wa wadhifa wa ubunge eneo bunge la Kilifi Kaskazini Amani Mkare.

Aidha, Mkare amewakata wazazi kuwahimiza watoto wao ambao wametiza umri wa miaka 18, kuchukua kadi za kura ili wawachague viongozi ambao watatekelezea miradi ya maendeleo.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.