Seneta Mteule Miraj Abdillahi amewataka viongozi wa pwani kushirikiana ili kufanikisha miradi ya maendeleo kwa wananchi badala ya kuendeleza siasa za chuki na migawanyiko miongoni mwa wenyeji.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa amesema hatua hiyo inadidimiza na kusambaratisha mshikamano wa wenyeji wa kaunti ya Mombasa.
Miraj amesema ni jambo la kusikitisha kuona viongozi hao wanaendeleza siasa ambazo hazina msingi badala ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Wakati huohuo ametoa wito kwa wenyeji kushirikiana na viongozi ambao wanapania kuwafanyia maendeleo na kujitenga na wale ambao wanaendeleza siasa za kuwagawanya..
Kauli yake imeungwa mkono na aliyekuwa mbunge Kisauni ambaye sasa ni Mwenyekiti wa bandari ya LAPSSET kaunti ya Lamu Ali Mbogo na kuwataka viongozi wa chama cha UDA kaunti ya Mombasa kushirikiana ili kukiimarisha.