VILABU VYOTE SITA VYA EPL VYAJIONDOA SUPER LEAGUE

Vilabu vyote sita vya ligi kuu ya uingereza vilivyokuwa vimekubali hapo awali kujiunga na ligi mpya ya super league vimejiondoa kutoka ligi hiyo iliyozua tumbo joto ulimwengu mzima miongoni mwa wakufunzi, wachezaji na mashabiki katika siku za hivi majuzi.

Huku klabu ya atletico Madrid na zile za italia AC Milan na Inter Milan zikijiondoa mapema hii leo Andrea Agnelli ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya Juventus lakini pia muanzilishi wa ligi hiyo ya European super league amesema kuwa na nikinukuu “itakuwa vigumu kwa mradi huo kuendelea baada ya vilabu vyote sita vya uingereza na viwili vya italia kujiondoa kutoka kwenye ligi hii”

Na kwengineko mmiliki wa klabu ya Liverpool John Henry kupitia vyombo vya habari na mitandao amewaomba radhi wachezaji wote, wakufunzi na mashabiki kwa kujihusisha na mradi huo wa super league ambao tayari ushafeli na kuahidi kuwa atafanya vyovyote kadri ya uwezo wake kuhakikisha anaboresha soka kwa ajili ya watu wote.

Na hatimaye klabu ya Manchester united imetangaza rasmi kuwa Ed Woodward ambaye ni naibu mwenye kiti wa klabu hiyo atakuwa anajihuzulu mwishoni mwa mwaka huu baada ya kuitumikia klabu hiyo ya manchester kwa miaka kumi na sita.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.