VIJANA NCHINI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJISAJILI KUWA WAPIGA KURA

Naibu Rais Daktari William Samoei Ruto amewataka vijana kujitokeza kwa wingi na kusajiliwa kuwa wapiga kura katika zoezi linaloendelea kwa mwezi mmoja.

Akizungumza jana baada ya kukutana na wawaniaji wa nyadhifa mbalimbali kutoka Mlima Kenya na Ukambani katika makazi yake mtaani Karen, Ruto amesema wakati umefika kwa wapiga kura kuwachagua viongozi ambao wamewajibika katika sera zao za maendeleo.

Ruto ambaye ameendelea kupigia debe sera yake ya kuinua uchumi wa wananchi wa mapato ya chini amesema mfumo huo utaondoa umasikini.

Amesema iwapo atashinda wadhifa wa urais 2022 atakahikisha suala la ajira linashughulikiwa pamoja na kuwapa wafanyabiashara wadogo mazingira bora ya kufanyia kazi ikiwemo kupata mikopo pamoja na kuwapa wakulima pembejeo ili waboreshe Kilimo nchini.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.