VIJANA KAUNTI YA KILIFI WALAUMIWA KWA VISA VYA MAUAJI YA WAZEE

Mwenyekiti wa  (MADCA) Emmanuel Munyaya, amesema  kwamba visa vya mauwaji ya wazee kaunti ya Kilifi vimeongezeka kwa kasi zaidi.
Haya ni kufuatia mauwaji ya wazee 20 waliouliwa huko Ganze kaunti ya Kilifi kwa tuhuma za uchawi ambapo Emmanuel ameeleza kwamba kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipinga maswala ya kitamaduni kwa madai kwamba yanahusiana na maswala ya kichawi na kupelekea wale wanaofuata tamaduni hizo kuwa wachawi.
Hata hivyo, amehoji kwamba kati ya sababu zinazochangia katika mauwaji hayo ni pamoja na baadhi ya vijana waliokataa kusoma kujiingiza katika uhalifu kwani hulipwa ili kutekeleza mauwaji hayo sambamba na kuwepo kwa  makundi yaliyoundwa kwa minajili ya kupinga tamaduni na kuyataja makundi hayo kuwa changizo kubwa.
Munyanya ameinyoshea serikali kidole cha lawama kwa kile alichokisema kuwa haijakuwa ikiangazia swala hilo na  kuwataka wakaazi kutojihusisha katika maswala hayo kwani ametaja kitendo hicho kama njia mojawapo ya kudhulumu haki za kibinadamu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.