USALAMA WA BAHARINI KUIMARISHWA KANDA YA PWANI

 

Katibu mkuu msimamizi katika wizara ya kilimo, Ufugaji na uvuvi nchini Lawrence Omuhaka amesema kwamba wanapania kuboresha usalama wa baharini ili kujenga mazingira bora ya wavuvi wa taifa hili ili kutekeleza shughuli zao za uvuvi bila matatizo yoyote.
Kwenye taarifa yake mjini Kilifi kaunti ya Kilifi Omuhaka amesema kwamba wavuvi wa taifa la Kenya wamekuwa wakihangaishwa wanapokuwa kazini ikiwemo kupokonywa vifaa vyao vya uvuvi.
Wakati uo huo Omuhaka amesema iwapo wavuvi watatumia vifaa vya kisasa na vilivyoidhinishwa wataweza kujiimarisha kiuchumi.
Naye Luciana Sanzua ambaye ni waziri wa kilimo katika kaunti ya Kilifi amewakosoa wavuvi ambao wamekuwa wakiwanyanyasa wanawake ambao wamekuwa wakiendeleza uchuuzi wa Samaki.

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.