USALAMA UTAIMARIKA LAMU KUTOKANA NA UJENZI WA BARABARA

Kamishna wa kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema kutokana na ujenzi wa barabara kuu kutoka kwenye bandari ya LAPSSET – IJARA – GARISSA – ETHIOPIA hadi Sudan Kusini usalama utaimaria kwa vijiji ambavyo viko kwenye msitu wa Boni.
Macharia anasema msitu wa Boni umekuwa ngome ya magaidi ambao wanaaminika kuwa Al- Shabaab na wamekuwa wakiutumia kujificha na kisha kutekeleza mashambulizi kwa wenyeji wa kaunti hiyo.
Tangu kuanzishwa kwa mradi huo hali imeanza kuwa tofauti na usalama kuanza kuimarika.
Naye mhandisi Ezekiel Fukwo ambaye ni naibu Mkurugenzi wa halmashauri ya usimamizi wa barabara kuu nchini keNHA amesema barabara yenye urefu wa kilomita 457 itajengwa kwa awamu tatu, Lamu –Ijara – Garissa kilomita 257, Bodhei – Basuba – Kiunga kilomita 113 na barabara ya Ijara – Sangailu – Hulugho kilomita 83.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *