UPANZI WA MIKOKO WAPANIA KUONGEZA IDADI YA MITI HIYO KAUNTI YA MOMBASA

 

 

Maadhimisho ya siku ya kutunza mikoko duniani yameandaliwa katika kaunti ya Mombasa huku wito ukitolewa kwa jamii kutokata mikoko kiholela.
Wanamazingira wakiongozwa na katibu mratibu katika wizara ya mazingira Mohammed Elim walikongamana katika fuo za Tudor Creek kwa maadhimisho hayo na kupanda mikoko.
Upanzi huo unapania kuongeza idadi ya mikoko na kukabiliana na kupungua kwa miti hiyo muhimu kwa viumbe walioko baharini.
Mohammed Elim pamoja na Julius Kamau wa shirika la utunzaji misitu nchini wamesema kuwa hamasisho la upanzi wa mikoko kwa wingi linatarajiwa kuongeza idadi ya miti hiyo eneo hilo la Tudor Creek.
Wakati uo huo wamesema mkondo wa bahari kanda ya pwani ni zaidi ya ekari elfu 10 na asilimia 40 zinadaiwa kuharibiwa na wanaojihusisha na pombe haramu.
Ukataji mikoko umechangia kupungua kwa viumbe walioko baharini kwa asilimia kubwa huku Maeneo ya Mshomoroni, Tudor na Mikindani yakidaiwa kuathirika zaidi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.