UONGOZI WA KAUNTI YA TAITA TAVETA WALAUMIWA

Makundi ya wachimba madini wadogowadogo eneo la Kishushe kaunti ya Taita Taveta wameushutumu uongozi wa kaunti hiyo kwa kile walichosema kuwa uongozi husika umekataa kuwawakea sahihi katika stakabadhi zao ili waweze kuchimba madini.
Wamesema kuwa kwa muda mrefu sasa wamekosa kunufaika kupitia raslimali ya madini katika eneo hilo kutokana na sababu zisizokuwa na msingi.
Wachimba madini hao wamesema kuwa machifu wamekosa kushirikiana nao katika kutatua swala hilo tata, wakisema kuwa maafisa hao tawala wamehujumu jitihada zao za kusajili makundi yao maarufu kama CBO.
Wakati uo huo wachimba madini hao wadogowadogo wameitaka serikali kupitia idara husika kuwaimarisha kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vya uchimbaji madini mbali na kuwatafutia soko ikizingatiwa kwamba kitega uchumi chao kikubwa kwenye eneo hilo ni madini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *