Ulaji wa Muguka wakithiri Kilifi

 

Mwenyekiti wa mradi wa kupambana na utumizi wa mihadharati, Anti Drugs Project ambaye pia ni Mwanaharakati wa kupambana na utumizi wa dawa za kulevya ukanda wa pwani Famau Mohamed Famau ametaja kukithiri kwa Muguka katika kaunti ya Kilifi na pwani kwa ujumla.
Famau amesema idadi kubwa ya vijana wamejiingiza katika makundi ya kihalifu sambamba na kusitisha masomo yao kutokana na utumizi wa bidhaa hiyo.
Wakati uo huo amehoji kando na vijana kutumia Muguka, wazee pia wamekuwa waraibu wa bidhaa hiyo hali ambayo imechangia kwa wao kutelekeza familia zao kutokana na kusahau majukumu yao.
Aidha Famau ameitaka serikali kupiga marufuku matumizi ya bidhaa hiyo hasa kwa vijana ili kunusuru kizazi kiijacho.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.