Ukarabati wa barabara zilizoharibika waanza Taita Taveta

 

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton samboja amesema bara bara zote ambazo ziliharibika baada ya kunyesha mvua zitakarabatiwa.

Samboja amesema sekta ya uchukuzi imeathirika pakubwa kutokana na hali hiyo na kuhoji kwamba tayari shughuli hiyo imeanza huku akisema baadhi ya barabara katika kaunti hiyo ziko chini ya serikali ya kitaifa na gharama yake ni ya juu zaidi.
Amewataka wabunge katika kaunti hiyo kuishinikiza serikali kuu kuzikarabati barabara hizo ili kuboresha swala la usafiri.
Hata hivyo amewahimiza wenyeji kuwajibika katika kuchangia kwenye maswala ya maendeleo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.